Hakumbuki ni siku ngapi za Ramadhaan alizoacha alipobaleghe


Swali:  Mimi ni mwanamke niliye na miaka arubaini. Nilipobaleghe utotoni sikufunga ile miezi ya kwanza ambapo nimekuja kuifunga hivi sasa na nimefunga miezi mine. Lakini nakumbuka kuwa nilibaleghe katika mwezi wa Ramadhaan na sikuufunga. Sikumbuki nilibaleghe mwanzoni mwake, katikati yake au mwishoni mwake. Niufunge mwezi huu vipi?

Jibu: Funga mwezi mzima. Maadamu jambo lenye lina uwezekano mbalimbali ambapo unadhani kuwa uliacha mwezi mzima, baadhi yake, siku nyingi au siku chache, lililo salama zaidi na linalotaka dhimma ni kufunga mwezi mzima.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 04/06/2017