Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye alifiliwa na mume wake na hakufanya eda kwa ujinga pamoja na kuzingatia kwamba kumeshapita muda mrefu?

Jibu: Hakuna kitu juu yake midhali ni mjinga. Lakini kuhusu kwamba mume wake alimwacha muda mrefu hakumzuii kufanya eda kama wanavofikiria baadhi ya watu. Baadhi ya watu wanasema mwanaume akimtaliki mke wake baada ya kuwa mbali naye muda mrefu basi hana eda. Akifa baada ya kumwacha kwa muda mrefu halazimiki kufanya eda. Haya ni makosa. Eda ni lazima kwa kila yule aliyekuwa na mume. Ni mamoja muda wa kupoteana umerefuka au hapana. Lakini akiacha eda kwa ujinga hakuna kitu juu yake. Kwa sababu imeisha kwa kuisha wakati wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (77) http://binothaimeen.net/content/1778
  • Imechapishwa: 20/09/2020