Hajj za wanawake pasina Mahram kwa kuchelea gharama


Swali: Mwanamke akisafiri peke yake pasina kuwa na Mahram kwenda Hajj, je, Hajj yake inakuwa sahihi? Kwa kuwa hivi sasa tunaona wanawake wengi katika mji wangu wanasafiri bila ya kuwa na Mahram na hilo ni kutokana na gharama za Hajj ikiwa ataenda na Mahram?

Jibu: Hajj yake ni sahihi ikiwa atatimiza masharti ya Hajj kikamilifu katika nguzo zake na mambo yake ya wajibu. Akiyatimiza haya Hajj yake ni sahihi. Lakini anapata madhambi kwa kuacha Mahram. Ni sahihi pamoja na kupata madhambi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-11-09.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014