Hajafunga Ramadhaan tatu kwa sababu ya kushika ujauzito kila Ramadhaan

Swali: Tokea miaka mitatu iliyopita mke wangu huzaa mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhaan na hajafunga miezi mitatu Ramadhaan. Ni ipi kafara?

Jibu: Ni wajibu kwake kuharakisha kulipa swawm ya Ramadhaan anayodaiwa ya miaka mitatu iliyopita kama ambavyo ni wajibu vilevile kulisha kwa kila siku masikini kiwango cha nusu ya Swaa´ katika ngano, mchele au chakula kilichozoeleka kuliwa katika mji. Hilo ni kwa sababu ya kuchelewesha kwake kulipa mpaka ikamwingilia Ramadhaan nyingine ikiwa Ramadhaan nyingine hiyo alikuwa ni muweza wa kuifunga.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/224)
  • Imechapishwa: 10/06/2017