Mtu ambaye anashikamana na Sunnah sahihi ambaye ndani ya moyo wake Sunnah imesimama imara, hawezi kukusanyika na mtu wa Bid´ah. Isipokuwa katika hali moja tu ikiwa hajui. Anakaa na mtu wa Bid´ah naye hajui. Anaweza kukaa nae hali ya kuwa hajui. Huyu ndiye aliyemkusudia Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah). Aliulizwa: “Je, nimkate mtu ambaye ni katika Ahl-us-Sunnah anatangamana na mtu katika Ahl-ul-Bid´ah? Akasema: “Hapana, mtahadharishe kwanza. Ukimuona baada ya hapo anatangamana nae mtie katika wao.”

Mtu katika Ahl-us-Sunnah anaweza kuwa hajui na khaswa pale ambapo atakuwa sio mkazi wa hapo au ni mji mpya au mzushi au Hizbiy mpya naye hamjui. Ni jambo linalowezekana kitu kama hichi kupitika hata kama atakuwa ni mwanachuoni. Mtu kama huyu atakumbushwa. Baada ya kukumbushwa, mtu ambaye ameshikamana kweli kweli na Sunnah sahihi hawezi kumkubali mtu ambaye anafuata Hawaa na Bid´ah.

Hali hii ya pili ndio khatari kwa mtu na ni msiba. Nayo ni kuwa, baada ya kutembea na kutangamana nao anachukua Bid´ah zao na kuwa kama wao. Na ndio maana kukasemwa rafiki husuhubiana. Ima ukasuhubiana nae wewe katika kheri au akasuhubiana na wewe katika shari. Na tofauti kati matangamano na nasaha iko wazi na kuna kizuizi cha wazi ambacho lazima mtu atanabahi nacho. Nasaha haihitajii matangamano.

Ikiwa baadhi yao wanadai kuwa anamnasihi Hizbiy huyu, mzushi au mtu anayefuata Hawaa, tunamwambia kuwa nasaha haihitajii matangamano. Hili ni jambo liko wazi. Unaweza kumnasihi katika kikao. Unaweza kumnasihi katika barua. Unaweza kumnasihi katika simu. Unaweza kumnasihi darsani. Lakini kusema wewe ukae nae na kutembea nae, hapana haiwezakani. Hii sio nasaha.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=38255
  • Imechapishwa: 20/01/2018