Swali: Je, inafaa kupungusa ndevu au kukata kitu humo? Kipi kinachomlazimu ambaye amefanya hivo?

Jibu: Haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Punguzeni masharubu na refusheni ndevu.”

“Jitofautisheni na washirikina.”

“Jitofautisheni na waabudia moto.”

Hadiyth ni zenye kuenea. Pia amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fugeni ndevu.”

“Ziacheni ndevu.”

“Zirefusheni ndevu.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 22/10/2021