Swali: Je, Muislamu ataadhibiwa akiwa na mapenzi ya kimaumbile kwa wazazi wake makafiri au mke wake wa Ahl-ul-Kitaab?

Jibu: Haifai kumpenda kafiri hata kama itakuwa ni mama yake, baba yake au kaka yake. Amesema (Ta´ala):

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ

“Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho [kuwa] wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa [ni] baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao.” (48:21)

Anatakiwa kumchukia kafiri chuki ya kidini na iwe kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Haijalishi kitu hata kama atakuwa mtu wa karibu zaidi kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_13.mp3
  • Imechapishwa: 19/06/2018