al-Halabiy amesema:

“Wapo na khaswa wanachuoni wakubwa Saudi Arabia ambao bado ni wenye kumsapoti na kumpendekeza Abul-Hasan na al-Maghraawiy. Je, hivi kweli muuliza au mjibiaji kusema kwa jumla ya kwamba fatwa hii kwa mtazamo huo ya kwamba elimu haichukuliwi kwa mwenye kufanya hivo? Hata kama itakuwa inahusiana na wanachuoni wakubwa? Sitaki kutaja jina lolote, lakini ni majina ya wanachuoni wakubwa ambao hawana mashaka yoyote na ni wenye kujulikana.”

Ndio. Ninasema wazi wazi ya kwamba haijuzu kuchukua elimu kutoka kwa mtu ambaye ana madhehebu ya Khawaarij. Haijalishi kitu ni nani. Kilichofanya tukasibiwa na hawa watu wenye kulipua, kukufurisha na kuharibu si kwa jengine isipokuwa ni kwa sababu wamechukua elimu kutoka kwa watu na vitabu vilivyo na madhehebu ya Khawaarij. Hili ni kosa dogo? Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema:

“Katika zama za mwisho watajitokeza watu wenye meno madogo na wapumbavu wa akili. Wanazungumza kwa maneno ya kiumbe bora kabisa, lakini wanatoka katika dini kama jinsi mshale unavyotoka kwenye upinda wake. Imani yao haivuki koo zao. Waueni popote mnapokutana nao. Yule mwenye kuwaua hakika ana ujira mkubwa siku ya Qiyaamah.”?

Kweli baada ya haya mtu anaweza kusema kuwa ni makosa mepesi? Au kwamba mtu asitahadharishe kuchukua elimu kwa mtu kama huyu?

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Durar an-Najmiyyah fiy Radd-ish-Shubuhaat al-´Aqadiyyah wal-Manhajiyyah, uk. 377-378
  • Imechapishwa: 18/03/2017