Swali: Kuna bwana mmoja anasema kuwa baadhi ya hukumu za dini zinahitajia kuangaliwa tena vizuri na kwamba zinahitajia kubadilishwa kwa sababu haziendani na maendeleo ya hivi sasa. Mfano wa hilo ni katika mirathi ambapo mwanamme anapata mfano wa fungu la wanawake wawili. Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwa mfano wa anayesema maneno kama haya?

Jibu: Hukumu ambazo Allaah amewawekea katika Shari´ah waja Wake na akazibainisha ndani ya Kitabu Chake kitukufu au kupitia kwa Mtume mwaminifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama mfano wa hukumu za mirathi, swalah vipindi vitano, zakaah, funga na nyenginezo, ambazo Allaah amewawekea wazi waja Wake na Ummah wakaafikiana juu yake, haifai kwa yeyote kupingana nazo wala kuzibadilisha. Kwa sababu ni usuniwaji uliopita juu ya Ummah katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baada yake mpaka kusimame Qiyaamah. Miongoni mwazo ni mtoto wa kiume kufanywa kuwa bora juu ya mtoto wa kike. Ni kitu ambacho Allaah (Subhaanah) amekiweka wazi ndani ya Kitabu Chake kitukufu na wakaafikiana juu yake wanachuoni wa waislamu. Kwa hiyo ni lazima kuyatendea kazi hali ya kuyaitakidi na kuyaamini. Ambaye atadai kuwa bora zaidi ni kinyume chake basi ni kafiri. Vivyo hivyo yule ambaye atajuzisha kwenda kinyume nayo pia ni kafiri. Kwa sababu ni mwenye kumpinga Allaah (Subhaanah), Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maafikiano ya Ummah. Kama ni muislamu basi ni lazima kwa mtawala kumtaka atubie. Vinginevyo basi italazimika kumuua hali ya kuwa kafiri aliyeritadi nje ya Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kubadilisha dini yake muueni.”

Tunamwomba Allaah atupe sisi na waislamu wote afya kutokamana na fitina zinazopotosha na kwenda kinyume na Shari´ah takasifu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/431)
  • Imechapishwa: 15/02/2021