Swali: Inajuzu mwa msafiri kuswali swalah ya ijumaa kwa aina ya swalah ya Dhuhr?

Jibu: Kama amehudhuria hapo basi aswali swalah ya ijumaa pamoja na waislamu. Asiswali Dhuhr.

Swali: Msafiri aliyeswali swalah ya ijumaa anaweza kuijumuisha na ´Aswr?

Jibu: Hapana, haifai kwa sababu swalah hizo mbili sio aina moja. Jengine ni kwa kuwa haikuthibiti ya kwamba Salaf walikuwa wakijumuisha ´Aswr pamoja na swalah ya ijumaa. Tumetafuta pasi na kupata kitu. Miaka kumi iliyopita kulitoka fatwa kwa muhuri wa Shaykh Ibn Baaz inayosema kuwa haijuzu kuunganisha ´Aswr pamoja na swalah ya ijumaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2017