1Mwenyezi Mungu akamwambia Mose na Aroni:

2Wawaambie Waisraeli hivi: 3Kati ya wanyama wote duniani, mmeruhusiwa kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua. 4Lakini msile mnyama yeyote ambaye hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili, au ambaye kwato zake zimegawanyika lakini hacheui. Msile ngamia, kwani hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili. Kwenu huyo ni najisi. 5Pelele msimle, yeye hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika; kwenu huyo ni najisi. 6Sungura msimle, yeye hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika; kwenu huyo ni najisi. 7Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi. 8Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Walawi 11:01-08
  • Imechapishwa: 12/01/2020