Ghafla kukata I´tikaaf


Swali: Kuna mtu anafanya I´tikaaf na anataka kwenda ´Umrah na baba yake. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ikiwa I´tikaaf inatokana nadhiri na imewekewa muda na wakati maalum, basi ni lazima aitekeleze. Kwa sababu kutekeleza nadhiri ya utiifu ni jambo la lazima. Ikiwa ni  I´tikaaf ya kujitolea tu, basi ataikamilisha na akitaka ataikata na kwenda ´Umrah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/446)
  • Imechapishwa: 12/06/2018