Swali: Kufanya fujo katika idadi ya chakula cha futari kunapunguza thawabu za swawm?

Jibu: Hakunpunguzi thawabu za swawm. Kitendo cha haramu baada ya kumaliza funga hakunpunguzi thawabu zake. Lakini hata hivyo hilo linaingia katika maneno Yake (Ta´ala):

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ

“Kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye hapendi wanaofanya israfu.” (07:31)

Israfu yenyewe imekatazwa. Uchumi ni nusu ya maisha. Ikiwa wako na neema basi waitoe swadaqah, kwani hilo ni bora.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/362)
  • Imechapishwa: 13/06/2017