Fir´awn alisema:

يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَ أَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا

“Ee Haamaan! Nijengee mnara ili nifikie njia. Njia za mbinguni ili nimchungulie Mungu wa Muusa, kwani hakika mimi namdhania ni mwongo.” (40:36-37)

Fir´awn anapinga kuwepo kwa Allaah [juu] kwa jeuri tu na wakati huo huo anajua ndani ya moyo wake ya kwamba Allaah yupo na kuwa Yeye ndiye mola wa ulimwengu huu. Amesema (Ta´ala):

وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا

“Wakazikanusha na hali kuwa nafsi zao zimeziyakinisha; kwa dhulma na majivuno.” (27:14)

Wenye kupinga uwepo wa Allaah na kwamba yuko mbinguni Fir´awn ndio kiongozi wao. Fir´awn ndio kiongozi wa Mu´attwilah ambao wanapinga kuwepo kwa Allaah mbinguni na kwamba amelingana juu ya ´Arshi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 10
  • Imechapishwa: 27/08/2020