Fataawaa za Kibaar-ul-´Ulamaa´ si kama za wengine

Swali: Gazeti la al-Iswlaah limeeneza fatwa ya Kibaar-ul-´Ulamaa´ inayozungumzia kufaa kufanya Tawassul kwa makaburi, waja wema  na Mitume baada ya kufa kwao na pengine umelisoma. Ni yepi maoni yako juu ya mambo kama haya? Ni yepi maelekezo yako juu ya kuraddi mfano wa shubuha kama hizi?

Jibu: Ikiwa jambo hili limethibiti na limenasibishwa kwao, basi mimi naona kuwa baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa´ Saudi Arabia wafikishiwe khabari na vilevile Muftiy Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah. Huenda kwa kufanya hivo baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa´ wataandika Radd dhidi ya taasisi hiyo ili haki iweze kubainika na kuwa wazi. Kwa sababu fatwa ikitoka katika baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa´ si sawa na kutoka kwa mtu wa kawaida.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 27/10/2019