Du´aa ya ulinzi dhidi ya vitu vinne ni katika swalah za faradhi peke yake?

Swali: Katika Tashahhud ya mwisho katika swalah ya sunnah tusome du´aa ya kuomba ulinzi kutokamana na vitu vine na du´aa nyenginezo au jambo hilo ni katika swalah ya faradhi peke yake?

Jibu: Isome katika swalah za sunnah na za faradhi. Sema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جهنم و من عَذَابِ الْقَبْر ومِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ وَ مِنْ شرِ فتنة الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ulinzi kutokamana na adhabu ya Moto, kutokamana na adhabu ya ndani ya kaburi, kutokamana na fitina ya uhai na kifo na kutokamana na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal.”

Tashahhud ya mwisho ni mahali pa du´aa katika swalah ya faradhi na ya sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… kisha achague du´aa zinazompendeza na aziombe.”

Aombe akitakacho katika mambo ya kidunia na Aakhirah muda wa kuwa ndani yake hamna madhambi wala kukata udugu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 02/11/2019