Swali: Mimi ni mwenye kumtendea wema baba yangu pamoja na hivyo mara nyingi ananiombea du´aa mbaya. Je, du´aa hiyo itanigusa?

Jibu: Ikiwa si mwenye kumkosea katika haki yake, du´aa yake dhidi yako haipokelewi. Ama ikiwa mwenye kumkosea katika haki yake, basi ni juu yako kujirudi na kutengeneza yale yaliyoko kati yako wewe na yeye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (82) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-08-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2018