Du´aa ndefu kwenye Witr


al-Fadhwl amesema:

“Nilisema kumwambia Abu ´Abdillaah: “Nifanye nini kama nataka kukhitimisha Qur-aan? Niiweke katika Witr au Tarawiyh? Madhumini ni sisi kuomba du´aa kati ya Rak´ah mbili.” Akasema: “Unapomaliza kusoma Qur-aan yote nyanyua mikono kabla ya Rukuu´ na uombe pamoja na sisi tumesimama katika swalah. Refusha du´aa.” Nikasema: “Niombe nini?” Akasema: “Unachotaka.” Nikafanya kama alivosema. Akasimama nyuma yangu na kuomba huku amenyanyua mikono.”

  • Mhusika: Imaam Abuul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Twabaqaat-ul-Hanaabilah (2/192)
  • Imechapishwa: 11/06/2017