Du´aa kwa lugha mbali na kiarabu ndani ya swalah

Swali: Je, inafaa kwa mwenye kuswali kuomba du´aa kwa lugha isiyokuwa ya kiarabu katika Sujuud au kwenginepo katika zile sehemu za swalah?

Jibu: Ndani ya swalah mnataka kuleta lugha ya kigeni? Kitendo hichi hakijuzu. Isipokuwa kwa ambaye hajui vizuri kiarabu. Ambaye hajui vizuri kiarabu aombe kwa lugha yake. Kuhusu ambaye anajua vizuri kiarabu haijuzu kwake kuomba kwa lugha nyingine ndani ya swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/12469
  • Imechapishwa: 18/01/2020