Swali: Miongoni mwa sababu za kuenea kwa uzinzi ni madereva na wafanyakazi kuwa wengi. Hayo yanaonekana vyuoni, katika masomo ya wasichana, masoko na minasaba mbalimbali. Ni yepi maelekezo yako? Je, inafaa kumwingiza nyumbani mfanyakazi msichana mdogo kwenye nyumba ambayo imejaa wavulana au kuwepo dereva pamoja na wasichana wenye umri mdogo. Tunaomba mwongozo.

Jibu: Haya hayahitajii mwongozo. Maelezo yenyewe yanatosha kuwa ni mwongozo. Hakuna mtu yeyote mwenye busara anayetaka jambo hili kabisa. Kwa sababu hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameharamisha mwanaume kuwa faragha na mwanamke. Amesema:

“Mwanaume hawi faragha na mwanamke isipokuwa watatu wao huwa ni shaytwaan.”

 Nasaha zangu juu ya wale wanaochukulia sahali jambo la faragha watubie kwa Allaah (´Azza wa Jall) na wasiwaache madereva wakawa faragha na wasichana. Utamuona mwanamke ambaye bado kijana akiwa pamoja na dereva ajinabi ambaye naye bado ni kijana. Ikiwa wewe baba unaweza kutangamana naye basi fanya hivo. Vinginevyo mwache aende na mmoja katika ndugu zake au awe pamoja na wanawake wengine wawili au watatu ili kuepuka jambo la faragha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1450
  • Imechapishwa: 01/01/2020