Chagua mwenyewe! – kufuata njia ya makafiri au ya Mtume wako (صلى الله عليه وسلم)?

Swali: Sisi siku zote tunakusanyika katika ukumbi wa mapumziko. Tuko na mtumzima mmoja hivi ambaye ananyoa ndevu zake kwa muendelezo. Tunapomwambia kwamba kunyoa ndevu ni haramu anapinga na kusema kwamba hakuna dalili ya wazi inayoharamisha. Anajadiliana nasi kwa maneno haya na sisi tunashindwa kumjibu kutokana na jinsi tunavyomuheshimu sana kwa sababu yeye ni mkubwa kuliko sisi. Kwa kuzingatia ya kwamba kanda hii ataisikia – kwa idhini ya Allaah – naye hivi sasa ameketi pamoja nasi katika kikao hichi. Sisi tunampenda na tunamfikiria.

Jibu: Allaah atujaze kheri sote. Kurudi katika haki ni fadhilah. Hapana shaka iwapo tutampa mtu khiyari ya kuchagua kati ya njia mbili; atachagua ipi kati ya njia ya waabudu moto na njia ya Mitume? Kila muumini atachagua mwenendo wa Mitume na katika kichwa chao yule wa mwisho wao; ambaye ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).  Wote walikuwa wakiachia ndevu. Upande mwingine waabudu moto ndio wananyoa ndevu. Chagua mwenyewe ni njia ipi unayotaka kupita!  Kwa ajili hii hatuoni kuwa kuna yeyote aliye na udhuru baada ya kumbainikia yeye haki kisha akaiacha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jitofautisheni na majusi, jitofautisheni na washirikina na ziacheni ndevu na yapunguzeni masharubu.”

Hii ndio desturi ya watu tokea hapo kale. Hatukuwa tunajua kuwepo kwa mwanaume yeyote anayenyoa ndevu zake. Bali walikuwa wanatwambia kwamba walikuwepo baadhi ya watawala wakandamizaji ambao walikuwa wanamuadhibu mtu kwa kuzinyoa ndevu zake. Wanafanya hilo ni kosa la kuadhibiwa. Wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wametaja katika kitabu cha taaziri kwamba haijuzu kumuazirisha mtu kwa kunyoa ndvu. Hiyo ni dalili kwamba baadhi ya watawala wakandamizaji walikuwa wakilitilia mkazo. Ni vipi basi mtu atapoteza pesa zake kwa  kujinyolesha? Kukhasirika zaidi ni kwa kule yeye kujikosesha kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutekeleza maamrisho yake. Tunataraji kwa ndugu yetu huyu ambaye mnamuheshimu Allaah (Ta´ala) amtunuku uongofu na aziachie ndevu zake kwa kutekeleza maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kufuata Sunnah yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (43) http://binothaimeen.net/content/985
  • Imechapishwa: 12/01/2019