Cha kufanya ada ya kila mwezi ikipitisha siku 15


Swali: Nilijiwa na ada ya mwezi na ikaendelea mpaka hivi sasa na kumeshapita siku kumi na mbili mpaka hii leo. Mwanamke huyu ada yake ni siku saba pekee. Hakuswali zile siku saba za mwanzo. Kisha baada ya hapo akaoga na akaswali kwa kujengea juu ya ada yake ya siku zote. Je, yale aliyofanya ni sahihi? Je, afunge au asifunge? Je, anahalalika kwa mume wake katika yale masiku mengine yaliyobaki?

Jibu: Kitendo chake huyu kingekuwa ni sahihi iwapo damu yake ingevuka siku kumi na tano. Ama kabla ya siku kumi na tano kuna uwezekano kuwa ada yake imezidi. Wakati fulani wanawake ada yao inaweza kuzidi na kupungua. Hivyo tunamwambia mwanamke huyu asubiri mpaka akamilishe siku kumi na tano. Baada ya kukamilisha siku kumi na tano ndipo uoge na uswali. Mwezi wa pili kaa siku zako tu. Kwa sababu si kweli kwamba mwanamke ni mwenye damu ya ugonjwa mpaka apitishe siku kumi na tano. Kukipita nusu ya muda basi ule wakati wake mwingi itakuwa ni damu. Hapo ndipo atarudi katika mazowea yake kabla ya kujiwa na ugonjwa huu. Si halali kwa mume wako mpaka kutimie siku kumi na tano. Baada ya hapo ndipo aoge na anakuwa halali. Kukija mwezi wa pili akae zile siku alizozowea kupata ada yake tu kisha aoge, aswali na ni halali kwa mume wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (69) http://binothaimeen.net/content/1556
  • Imechapishwa: 26/02/2020