Bora siku kumi za Ramadhaan au za Dhul-Hijjah?


Swali: Bora ni yale masiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan au yale masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah inapokuja katika matendo mema?

Jibu: Wanazuoni wamesema kuwa ile michana kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah ni bora kuliko michana kumi ya mwisho ya Ramadhaan. Na nyusiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan ni bora kuliko nyusiku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/05_20.mp3
  • Imechapishwa: 07/07/2021