Swali: Bora kwa aliyedhulumiwa ahifadhi yake kwa ajili ya siku ya Qiyaamah na asimsamehe mgombezi wake duniani kwa sababu atakuwa ni mwenye haja ya matendo mema siku ya Qiyaamah au bora zaidi ni kusamehe?

Jibu:

وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِّثْلُهَا ۖ فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ

“Na jazaa ya uovu ni uovu mfano wake. Lakini anayesamehe na akasuluhisha, basi hakika ujira wake uko kwa Allaah.” (42:40)

Bora zaidi ni kusamehe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2107
  • Imechapishwa: 01/07/2020