Bora kuoa mke mmoja au wengi?     

Swali: Kuna mwanaume ana uwezo wa kimali na wa kimwili. Je, bora kwake kuoa mke mmoja peke yake au kuoa wake wengi?

Jibu: Kuoa wanawake wengi ndio bora zaidi kuliko kuoa mke mmoja tu. Hilo ni kwa sababu ya kule kukithirisha kizazi katika Ummah huu na kutokana vilevile na kuzihifadhi tupu za wanawake ambao hawana waume. Hilo ni kwa sharti zifuatazo:

1- Mtu awe na uwezo wa kimali.

2- Uwezo wa kimwili.

3- Uwezo wa kuitendaji. Namaanisha kuwafanyia uadilifu wanawake. Ama kuoa tu ilihali anachelea hatokuwa mwadilifu, hilo ni haramu juu yake. Allaah (Ta´ala) anasema:

فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً

“Mkichelea kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi bakini na mmoja tu… “

Katika hali hii Allaah ameamrisha kubaki na mke mmoja tu.

أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ

“… au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki.” (04:03)

Wanawake kama hawa – yaani masuriya – sio wajibu kufanya uadilifu kati yao. Anaweza kulala na amtakaye katika wanawake hawa – ikiwa yuko nao – na sio wajibu kufanya uadilifu. Kuhusu wake ni lazima kuwafanyia uadilifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
  • Imechapishwa: 03/05/2020