Katika Sunnah imekuja ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwabashiria Maswahabah wake juu ya kuja kwa mwezi huu. Imekuja katika Hadiyth ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaambia Maswahabah wake:

“Umekujieni mwezi wa Ramadhaan, mwezi wa baraka. Allaah amekufaradhishieni swawm yake. Ndani yake hufunguliwa milango ya Pepo, hufungwa milango ya Moto na mashaytwaan hufungwa minyororo. Ndani yake kuna mwezi ambao ni bora kuliko miezi elfumoja. Atayenyima kheri zake hakika huyo amenyima.” Ahmad (7148), (8991) na (9497), an-Nasaa´iy (2106).

Hii ni bishara na hongera kwenu. Anawajulisha jambo kubwa lililowafikia. Nalo si lingine ni kwamba Ramadhaan imewajia hali ya kuwa mna siha na afya njema, mnaneemeka kwa usalama, amani na Uislamu. Huu ni mwezi wa Ramadhaan ulokujieni. Huu mwezi ambao ni msimu mkubwa wenye kutumiwa kumkimbilia Allaah, kuihesabu nafsi, kumtii Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na kujitenga mbali na mambo aliyoharamisha Allaah (Jalla wa ´Alaa).

Maneno haya yanazitikisa nyoyo ili ziweze kuhisi hadhi, nafasi na ukubwa wa manzilah ya mwezi huu. Kwa msemo mwingine anachotaka kusema ni kwamba jiandaeni juu ya kuja kwake na ukaribisheni vizuri kabisa.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Wa jaa´ Sharh Ramadhwaan, uk. 06-07
  • Imechapishwa: 19/05/2020