Swali: Je, kila anayetumbukia katika Bid´ah anaitwa mzushi?

Jibu: Ni jambo linalojulikana kwamba Bid´ah ni zenye kutofautiana. Lakini kuilenga Bid´ah na kuifanyia mpaka watu wanatofautiana ndani yake. Lakini  zipo Bid´ah ambazo ziko wazi na jambo lake liko wazi. Kama inavyojulikana watu wanatofautiana katika Bid´ah hizi. Kwa hiyo haisemwi kuwa Bid´ah zote zinalingana. Lakini watu wameafikiana kwamba zote ni zenye kwenda kinyume na Shari´ah, kwamba zinakwenda kinyume na mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ijapokuwa zinatofautiana. Haisemwi kwamba zote ziko katika kiwango kimoja. Ni kama ambavyo dhambi na maasi haziko katika kiwango kimoja. Dhambi kubwakubwa haziko katika kiwango kimoja. Vivyo hivyo kuhusu Bid´ah haziko katika kiwango kimoja.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 09/11/2019