Biashara ya mnada


Swali: Je, inazingatiwa kuwa ni biashara ya mnada iliyokatazwa ambapo mtu anaongeza juu ya zabuni ya ndugu yake?

Jibu: Inategemea. Ikiwa mnada bado unaendelea na bidhaa inaendelea, basi hakuna neno ukapandisha zabuni yako juu ya mwingine. Kwani lengo ni kuongeza zabuni na mnada bado unaendelea. at-Tirmidhiy amepokea kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaweza kusema katika baadhi ya biashara:

“Ni nani ambaye atazidisha?”

Ama ikiwa mnada umekwisha, zabuni imekwishapita na muuzaji akajaribu kumuuzia mteja mwingine, basi hapo haifai kwa yeyote kuinunua na hivyo akanunua mbele ya ndugu yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… na wala asitoe zabuni juu ya zabuni ya ndugu yake.”[1]

[1] al-Bukhaariy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://ar.islamway.net/fatwa/9581/%D9%87%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B2%D8%A7%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%84%D9%86%D9%8A-%D9%8A%D8%B9%D8%AA%D8%A8%D8%B1-%D9%85%D9%86-%D8%B4%D8%B1%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AC%D9%84-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%B4%D8%B1%D8%A7%D8%A1-%D8%A3%D8%AE%D9%8A%D9%87
  • Imechapishwa: 21/02/2021