Bakora wakati wa Khutbah kwa mujibu wa Ibn Baaz

Swali: Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema kuwa haikuhifadhiwa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akipanda juu ya mimbari na bakora, silaha ya mshale wala kitu kingine. Wala kwamba kabla ya kuishika kwamba alikuwa anashika upanga na kwamba alikuwa akiegemea kwenye bakora na silaha ya mshale. Kinachopata kufahamika kutoka kwenye maneno yake (Rahimahu Allaah) ni kwamba kushika bakora wakati wa Khutbah ni jambo halikuthibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kupanda juu ya mimbari. Je, ni sahihi?

Jibu: Cheni ya wapokezi imetaja bakora au mshale. Imekuja vilevile katika Hadiyth al-Hakam bin Hazm ya kwamba alimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakhutubia watu na huku akiegemea juu ya bakora au silaha ya mshale. Jambo hili lina wasaa ndani yake. Si kwamba ni jambo limekokotezwa sana au kwamba ni wajibu. Khatwiyb akishika mkononi mwake kitu hakuna neno na akikhutubu pasi na mkononi mwake kuwa kitu hakuna neno. Kinacholengwa ni kwamba kushika mkononi mwake bakora, upanga au kitu kingine hakuna neno. Hili linakuwa wakati wa Khutbah. Si kwamba ni jambo limekokotezwa. Bali alilifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ilivyo katika Hadiyth ya al-Hakam. Kitendo chake kuna uwezekano kilijitokeza kwa haja tu kama ambavyo vilevile kuna uwezekano alifanya hivo kwa sababu ya kubainisha Sunnah. Hivyo mwenye kufanya hivo ni sawa na asiyefanya hivo pia ni sawa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2928/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D8%AA%D8%AE%D8%A7%D8%B0-%D8%B9%D8%B5%D8%A7-%D8%A7%D8%AB%D9%86%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%AE%D8%B7%D8%A8%D8%A9
  • Imechapishwa: 26/01/2019