Baadhi ya sababu za kuwa imara juu ya haki


Swali: Mimi ni kijana mwenye msimamo – himdi zote ni za Allaah – na ninakhofia kupotea. Ninaomba unipe nasaha.

Jibu: Ndio, sote tunakhofia. Hakuna yeyote mwenye kujiaminia. Mtu akikhofia kupotea ni dalili ya imani yake na kumuogopa kwake Allaah (´Azza wa Jall) na kwamba hajiaminishi nafsi yake na kuitakasa.

Lakini ni juu yako kushikamana na wanachuoni, watu wa haki, kukaa na wanachuoni na kuhudhuria durusi za elimu yenye manufaa. Ni juu yako kushikaman na hayo. Lazimiana na vikao vya elimu na ustafidi navyo. Soma vitabu vyenye manufaa. Sikiliza barnamiji zenye manufaa zinazorushwa kwenye idhaa an-Nuur ´alaad-Darb na kisomo cha Qur-aan Tukufu. Hizi ni miongoni mwa sababu za kuwa na uimara katika haki na uongofu. Vilevile kithirisha matendo mema na kuomba Du´aa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_15.mp3
  • Imechapishwa: 12/06/2018