Baadhi ya madhara ya TV


TV ni kifaa cha khatari na madhara yake ni makubwa kama vile sinema au baya zaidi. Tumeijua kupitia vijitabu vilivyoandikwa juu yake na kupitia wale wenye kuitambua katika miji ya kiarabu na mingineyo mambo yanayofahamisha juu ya ukhatari wake na madhara yake mengi kwa ´Aqiydah, tabia na hali za jamii. Hayo ni kutokana na zile filamu mbaya zinazorushwa ndani yake, maono yenye kufitinisha, picha za uchi au nusu uchi, Khutbah zenye kuangamiza, makala za kufuru, mashaji´isho juu ya kujifananisha na makafiri katika tabia zao na viongozi wao na kuwaadhimisha wakuu wao na viongozi wao. Sambamba na hilo inapuuzilia mbali tabia na sera za waislamu, kuwadharau wanachuoni wa waislamu na mabingwa wa Uislamu, kuubatilisha Uislamu, kuwaonyesha kwa sura inayowafanya watu kukimbia mbali nao, yanayopelekea kuwadharau na kupuuzilia mbali historia yao, inabainisha njia za vitimbi, ulaghai, uharibifu, uibizi, wizi na kuwafunza watu namna ya kuwa na uadui kwa watu wengine.

Hapana shaka kitu chenye sifa hizi na kinapelekea katika uharibifu uliotajwa basi ni wajibu kukizuia, kutahadhari nacho na kufunga milango inayopelekea huko.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/articles/84/%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AF-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D8%AA%D9%87%D8%A7%D9%85%D8%A7%D8%AA-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%85%D8%B1%D9%8A%D9%86-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B9%D8%B1%D9%88%D9%81-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%B4%D8%AF%D8%AF
  • Imechapishwa: 07/10/2018