Swali: Mimi nafanya kazi hospitalini. Ni vipi nitashikamana na msimamo ilihali ni mtaalam katika kitendo cha wanawake?

Jibu: Kwa hali yoyote unaweza kushikamana na msimamo kwa kiasi cha vile unavoweza. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ

“Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika dini.”[1]

Usiwalegezee sauti wanamme, usiwe faragha na mwanamme yeyote, usimwonyeshe uso wako isipokuwa kwa yale haja itapelekea kufanya hivo na hapo ikibidi uonyeshe jicho moja ambalo utaweza kuona kwalo na ushikamane na [maamrisho mengine] aliyoamrisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaamrisha wanawake wa waumini. Afanye vile atavyoweza na tunamuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ailete siku ambayo kutakuwa na hospitali za wanawake peke yao na wanamme peke yao – kwani hilo kwa Allaah si jambo lenye kushindikana. Tunamuomba Allaah aiwafikishe serikali yetu kulifanya hilo ili kusalimike na uvumi na ili vilevile wale wanawake walioshikamana na dini waweze kusalimika na dhambi ambazo wanaweza kutumbukia.

[1] 22:78

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (39) http://binothaimeen.net/content/886
  • Imechapishwa: 01/06/2020