Hivyo Tawassul kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imegawanyika ifuatavyo:

1- Kutawassul kwa kumuamini. Hili ni sawa.

2- Kutawassul kwa du´aa yake na siku ya Qiyaamah. Hili pia linajuzu.

3- Kutawassul kwa dhati yake. Hili limekatazwa.

Kuhusiana na Hadiyth ya kipofu ambapo alisema:

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba na kuelekea Kwako kupitia kwa Muhammad ambaye ni Mtume wa Rahmah. Mimi naelekea [nakuomba kupitia] kwako kwa Mola Wangu ili anirudishie macho yangu. Ee Allaah! Mshufaie kwangu.” at-Tirmidhiy (3578).

Sahihi ni kwamba kipofu alitawassul kwa du´aa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiomba du´aa na yeye anaitikia “Aamiyn”.

Hivyo kutawassul kwa dhati, kutawassul kwa jaha kama kwa mfano kusema “Ninatawassul kwa jaha ya fulani”, “Haki ya fulani”, “Heshima ya fulani”, haya yamekatazwa na ni Bid´ah. Tawassul ya Kishari´ah inakuwa:

Mosi: Kwa du´aa ya mtu aliye hai na yuko mbele yako. Kwa mfano yeye anaomba na wewe unaitikia “Aamiyn”.

Pili: Kutawasssul kwa kumuamini Allaah, Mtume Wake na Tawhiyd yake.

Tatu: Kutawassul kwa matendo yako mema. Kama walivotawassul wale watatu waliongia pangoni na mlango ukawa umejifunga. Mmoja wao akatawassul kwa kuwatendea wazazi wake wema, wapili akatawassul kwa kujiepusha kwake na uzinzi na watatu akatawassul kwa uaminifu wake. Tawassul sampuli hizi ni sawa. Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ

“Hakika mimi ni mhitajia wa kheri yoyote Utakayoniteremshia.” (28:24)

Unaweza kutawassul kwa ufakiri na kule kumuhitajia kwako Allaah au kwa Majina na sifa Zake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/332-333)
  • Imechapishwa: 21/05/2020