ar-Raajihiy kuhusu kufuru na shirki


Swali: Je, kufuru na shirki vinaingia katika kanuni isemayo:

“Vikikutana basi kila kimoja kinakuwa na maana yake na vikiachana kimoja kinakuwa na maana ya kingine.”?

Jibu: Kufuru ndio shirki na shirki ndio kufuru. Kafiri ambaye anapinga kupwekeshwa Allaah ni mshirikina kwa sababu ameabudu matamanio na amemuabudu shaytwaan. Mshirikina pia ni kafiri kwa sababu amepinga kupwekeshwa kwa Allaah na amepinga haki Yake. Lakini mshirikina ikiwa kufuru yake ni kwa upande wa ukanushaji ni jambo khafifu ukilinganisha na kufuru. Shirki yake ikiwa kwa upande wa kuabudu asiyekuwa Allaah basi inakuwa khafifu kidogo kuliko shirki. Vinginevyo kila mshirikina ni kafiri na kila kafiri ni mshirikina.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 05/02/2018