´Aqiydah ya maimamu wanne


Miongoni mwa jumla ya Salaf-us-Swaalih waliyokuwa juu ya I´tiqaad thabiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na Taabi´uun ni maimamu wane; Imaam Abu Haniyfah, Imaam Maalik, Imaam ash-Shaafi´iy, Imaam Ahmad na maimamu wengine ambao walisimama kidete kuitetea ´Aqiydah, kuilinda, kuibainisha na kuwafundisha nayo wanafunzi.

Maimamu wane walikuwa wakiitilia umuhimu ´Aqiydah hii, wakiifundisha na wakiwahifadhisha nayo wanafunzi zao na watoto wao. Wameandika vitabu vingi kuhusu ´Aqiydah juu ya mfumo wa Qur-aan na Sunnah na ufahamu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake na Taabi´uun na wakati huo huo wanaraddi ´Aqiydah batili na potevu na wakabainisha upindaji na upotevu wake.

Kadhalika maimamu wa Hadiyth; kama Ishaaq bin Raahuuyah, al-Bukhaariy, Muslim, Imaam Ibn Khuzaymah na Imaam Ibn Qutaybah. Vilevile maimamu wa tafsiri, kama mfano wa Imaam at-Twabariy, Imaam Ibn Kathiyr, Imaam al-Baghawiy na wengineo katika maimamu wa tafsiri.

Wameandika vitabu vingi kuhusu hili. Mwanzoni walikuwa wakiviiita “as-Sunnah”. Kwa mfano “as-Sunnah” cha Ibn Abiy ´Aaswim, “as-Sunnah” cha ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal, “as-Sunnah” cha al-Khallaal, “as-Shari´ah” cha al-Aajurriy na vinginevyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-it-Twahaawiyyah, Uk. 25-26
  • Imechapishwa: 05/09/2020