´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya Yaziyd bin Mu´aawiyah

Swali: Ni ipi ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya Yaziyd bin Mu´aawiyah?

Jibu: ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya Yaziyd bin Mu´aawiyah ni kwamba alikuwa mtawala miongoni mwa watawala wa waislamu. Ana mazuri yake na mabaya yake ambayo Allaah ndiye atamuhukumu kwayo. Hayo yamesemwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) na wengineo. Yeye ni miongoni mwa watawala wa waislamu ambaye ana mazuri na mabaya yake. Yeye ni miongoni mwa wapwekeshaji na hakuwa kafiri. Allaah (Ta´ala) ndiye ambaye atasimamia jambo la hesabu kati ya waja Wake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/13/%D8%B9%D9%82%D9%8A%D8%AF%D8%A9-%D8%A3%D9%87%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%B3%D9%86%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D9%8A%D8%B2%D9%8A%D8%AF-%D8%A8%D9%86-%D9%85%D8%B9%D8%A7%D9%88%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 11/01/2020