Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hakuna aliyesalimika katika dini yake isipokuwa yule aliyejisalimisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akairudisha elimu ya yale yenye kumtatiza kwa mwenye kuyajua.”

Mambo ni kama alivosema Shaykh (Rahimahu Allaah). Hakuna yeyote aliyesalimika katika dini yake isipokuwa yule aliyejisalimisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa maandiko ya Kishari´ah ambayo ni Qur-aan na Sunnah.

Lililo la wajibu ni kujisalimisha kikamilifu kwa Allaah na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kurudisha elimu ya yale yenye kutatiza kwa mwenye kuyajua. Asipingane na maandiko ya Qur-aan na Sunnah kwa kuyatilia shaka, utata na tafsiri mbovu. Kwa mfano akasema “Andiko hili haliingii akilini mwanangu na andiko ndio mapokezi asli. Hivyo andiko likipingana na akili sisi tunatanguliza akili mbele.” Hii ni batili kubwa kabisa.

Lililo la wajibu ni kujisalimisha kwa Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa maandiko ya Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/267)
  • Imechapishwa: 23/05/2020