Swali: Mwenye kuvaa soksi kwenye mguu wake wa kulia kabla ya kuosha mguu wake wa kushoto…

Jibu: Asifute juu yake mpaka azivae akiwa katika hali ya twahara, kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). al-Mughiyrah amesema:

“Siku moja wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anatawadha, nikakimbia ili nimvue soksi zake za ngozi. Ndipo akasema: “Ziache, hakika mimi nilizivaa nikiwa na twahara.” Kisha baada ya hapo akapangusa juu yake.”

Miguu haijakuwa na twahara akivaa soksi moja kabla ya kuosha mguu mwingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (17) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtf-08011435.mp3
  • Imechapishwa: 27/10/2019