Swali: Baadhi ya watu waliopo wanatukufu pamoja na washirikina kwenye makaburi na huku wanadai kwamba wanafanya hivo ili wawapende. Kisha baada ya hapo ndipo wanawalingania kuacha kutufu huku. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi?

Jibu: Mwenye kutufu pamoja nao basi amefanya matendo yao na kuafikiana nao. Hili litakuja katika kitenguzi cha tatu. Yule asiyewakufurisha washirikina au akawa na mashaka juu ya ukafiri wao, linakuja huko mbele. Haijuzu kwa muislamu kushirikiana na washirikina katika matendo yao na akatukufu pamoja nao kwenye makaburi kwa sababu ya kuwapaka mafuta, kuwaridhisha na kutowakemea. Hili halijuzu. Huu sio mfumo wa kulingania kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 76
  • Imechapishwa: 30/08/2018