Anataka kurudi mwanzo swalah ambayo hakunyenyekea

Swali: Anayesoma Suurah katika swalah – ni mamoja al-Faatihah au nyingine – na akahisi mwishoni mwake kuwa hakufanya unyenyekevu ndani yake. Je, inafaa kwake kuirudia?

Jibu: Hapana. Ajitahidi katika Rak´ah au swalah zilizosalia kuzinduka kuanzia mwanzo wake. Asijifungulie mlango wa wasiwasi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 153
  • Imechapishwa: 03/07/2022