Anataka kurudi kulala Minaa

Swali: Mtu mwenye kutoka Minaa tarehe 12 kisha akataka kurudi kulala huko. Je, inafaa kwake kufanya hivo?

Jibu: Kama amerudi hajj yake imekwisha. Inafaa kwake kurudi na akalala pamoja na marafiki zake au kama anataka kutekeleza haja yake fulani, lakini asirushe vijiwe katika siku ya tarehe 13. Kwa sababu ametoka Minaa mapema na hivyo mambo yamekwisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 31/05/2020