Anataka kumleta mama nyumbani lakini mke hataki


Swali: Mama yangu anaishi katika nyumba peke yake na anasumbuka sana kwa sababu ya jambo hilo. Hivyo nikataka kumleta ili aishi nasi katika nyumba yangu. Lakini hata hivyo mke wangu amekataa jambo hilo na nimejaribu njia mbalimbali nzuri ili kumkinaisha. Lakini pasi na mafanikio. Je, nimtaliki mke wangu kwa sababu hiyo?

Jibu: Hili lahitajia kutazamwa kwa njia mbalimbali:

Mosi: Je, mama ameng´ang´ania mtoto wake amuhamishe nyumbani kwake?

Pili: Je, mke huyu kishazaa naye watoto kwa njia ya kwamba akimpa talaka watoto watatawanyika na kutatokea uharibifu kwa sababu hiyo?

Tatu: Je, anaweza kukodi nyumba jirani yake na akamweka mama yake ndani yake na akaweka mlango kati yake yeye na mama yake ambapo kila mmoja anaweza kuingia kwa mwenzake? Ikiwa hili linawezekana basi ndilo la lazima. Siwezi kukwambia kwamba umpe talaka mke wako. Kwa sababu nachelea kwamba mama hajakulazimisha jambo hilo. Ametulia juu ile hali aliyomo na hajali. Jengine nachelea ni kwamba kumtaliki mke kukapelekea watoto kutawanyika na kukapatikana madhara makubwa. Namuomba Allaah (Ta´ala) amkusanye kati yake, mama yake na mke wake juu ya njia iliyonyooka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (68) http://binothaimeen.net/content/1537
  • Imechapishwa: 18/02/2020