Anaswali Sunnah baada ya kukimiwa swalah

Swali: Tunaona baadhi ya watu wanapoingia msikitini kwa ajili ya kuswali Fajr na kumeshakimiwa swalah basi wanaswali Rak´ah mbili za Fajr kisha baadaye wanajiunga na imamu. Ni ipi hukumu ya hilo? Je, bora mtu aiswali moja kwa moja baada ya Fajr au asubiri mpaka lichomoke jua?

Jibu: Haijuzu kwa ambaye ameingia msikitini na kumeshakimiwa swalah akaswali Rak´ah mbili za mamkuzi ya msikiti au Raatibah ya msikiti. Bali ni lazima kwake kujiunga pamoja na imamu katika ile swalah inayoswaliwa hivi sasa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kunapokimiwa swalah basi hapana swalah nyingine isipokuwa ile ya faradhi.”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

Hadiyth hii inakusanya swalah ya Fajr na nyinginezo.

Aidha ni mwenye kupewa khiyari; akitaka anaweza kuswali Raatibah baada ya swalah na akitaka anaweza kuichelewesha mpaka baada ya kuchomoza kwa jua na ndio bora zaidi. Kwa sababu imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanayojulisha mambo yote mawili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/372)
  • Imechapishwa: 16/08/2022