Anasafiri na mama na shemeji


Swali: Mwanamke anasafiri na mama yake na mume wa dada yake. Huku kunzingatiwa ni kusafiri bila Mahram?

Jibu: Ndio. Asisafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram:

“Si halali kwa mwanamke anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho akasafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 08/09/2018