Anahisi wudhuu´ kutenguka wakati anatawadha na swalah

Swali: Wakati mwingine niko natawadha nahisi kuwa wudhuu´ unatenguka na pia ndani ya swalah. Sijui kama ni jambo la kihakika au ni wasiwasi. Jambo hili limenifanya kukosa swalah ya mkusanyiko. Unaninasihi nini?

Jibu: Ninakunasihi uache wasiwasi. Huu ni wasiwasi. Achana nao. Ukihisi hayo mtake ulinzi Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa na yapuuze. Endelea na wudhuu´ wako na swalah yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%204%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2017