Anaenda kwenye duka jirani kumnunulia mteja wake bidhaa

Swali: Mtu akiniomba bidhaa fulani ambayo sina ambapo nikamwambia kuwa nitamletea baada ya saa moja. Nikatoka na kumletea bila kuchukua malipo yoyote kutoka kwake na mkataba ukakamilika baada ya hapo. Je, biashara hii ina makatazo upande wa Shari´ah?

Jibu: Bidhaa unatakiwa uimiliki wewe kwanza na na mteja awe khiyari kuichukua au kutoichukua. Inatakiwa iwe katika umiliki wako kwanza. Ama kuamua wewe na yeye akaamua kwamba atainunua ilihali bado hajaiona na ukamwambia kuwa itakuwa juu ya dhimma yake baada ya kumnunulia nayo ni kitu kisichojuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 19/04/2021