Ametukufu Twawaaf-ul-Wadaa´ kisha akalala

Swali: Nilihiji faradhi ya hajj na baada ya kumaliza Twawaaf-ul-Wadaa´ nikalala Makkah kwa sababu nilikuwa nimechoka sana. Sikuamka isipokuwa siku ya pili. Je, juu yangu kuna kinachonilazimu?

Jibu: Ni lazima kwake kuirudi Twawaaf hiyo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiondoke yeyote mpaka iwe kitendo chake cha mwisho ni Twawaaf.”[1]

Haya ni miongoni mwa maneno yake ya mwisho kabisa kabla ya kufariki. Ni lazima kwake kurudi kutufu. Ikiwa hakufanya hivo, basi naona kwamba ni salama zaidi ni yeye kuchinja fidia Makkah na awagawie mafukara.

[1] Ameipokea Muslim na wengineo. al-Bukhaariy amepokea mfano wake. Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (1086) na Swahiyh Abiy Daawuud” (1747).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1413
  • Imechapishwa: 15/12/2019