Swali: Chuoni kunaadhiniwa kwa ajili ya swalah ya Dhuhr ambapo naiswali nikiwa na janaba. Kwa sababu mbele ya mamia ya wanafunzi na waalimu inaniwia vigumu kuwaambia jambo hili na hilo sio kwa sababu ya kuhisi kwangu uvivu. Nalala baada ya Fajr na naamka nimechelewa ambapo nalazimika kwenda shuleni. Ninaporudi nyumbani ndio hujisafisha na kuswali.

Kuna mwingine anasema asubuhi ya kwanza kambini niliamka na nikajikuta niko na janaba. Hiyo ilikuwa janaba ya sita ndani ya siku sita. Je, hayo ni maradhi au ni kitu gani? Je, nalazimika kuoga pamoja na kuzingatia kwamba hakuna sehemu za kuogea katika maeneo hayo?

Jibu: Kuswali hali ya kuwa na janaba ni miongoni mwa madhambi na maovu makubwa. Akifanya hivo kutokana na uchache wa kujali na kuifanyia dhihaka Shari´ah, jambo lake lake ni khatari mno. Anaweza kuritadi kutoka nje ya Uislamu ikiwa anacheza shere na kuidharau Shari´ah. Tunacholenga ni kwamba jambo hilo ni khatari sana.

Ni lazima mtu kutahadhari kutokamana na hilo asiswali akiwa na hadathi. Tusemeje kuswali akiwa na janaba?

Kwa hivyo ni lazima kutahadhari. Ikiwa kule anakoenda hakuna sehemu ya kuogea basi analazimika kufanya haraka kabla ya kutoka ijapo atachelewa. Kabla ya kutoka mahala pake aoge ijapo atachelewa kazini kwake au shuleni. Hayo ni yenye kutangulizwa mbele ya masomo, kazi na mambo mengine yote. Akitozwa pesa jambo ni sahali. Haijuzu kwake kabisa kutoka mahale pake ilihali ana janaba. Isipokuwa ikiwa kule mahali anapoenda kuna sehemu ya kuogea. Mbaya na kubwa zaidi kuliko hilo ni yeye kuswali akiwa na janaba. Huu ni uovu mkubwa, uharibifu mkubwa na kuchukulia wepesi amri ya Allaah. Lakini akifanya hivo kwa kejeli na dharau ni ukafiri. Amesema (Ta´ala):

قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Sema:  Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?”  Msitoe udhuru; mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (09:65-66)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4281/حكم-من-صلى-على-جنابة-حياء-من-الناس
  • Imechapishwa: 15/06/2022