Ameshtuka baada ya kupita miyqaat


Swali: Nilipanda ndege nikiwa na mavazi ya Ihraam na nikajitia manukato. Wakati nilipokuwa nasubiri ndege itangaze kuwa tumefika miyqaat nikapitiwa na usingizi na sikuamka isipokuwa baada ya ndege kutua. Kipi kinachonilazimu?

Jibu: Ulifanya nini pindi ulipoamka? Ni wajibu kwako kurudi miyqaat. Hukunuia Ihraam. Rudi miyqaat na uhirimie kutoka hapo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (70) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighatsah%20-%2019%20-0%207%20-%201438.mp3
  • Imechapishwa: 10/09/2017