Amesahau akaingia chooni na Qur-aan


Swali: Vipi mtu akiingia chooni na akasahau kuwa mfukoni mwake ana msahafu au Qur-aan ilio na msahafu?

Jibu: Hakuna neno juu ya hilo midhali Qur-aan hiyo iko mfukoni mwake na ameifunika na kufichikana. Hakuna neno juu ya hilo. Lakini bora zaidi ni yeye asiingie bafuni au sehemu ya kukidihia haja na kitu kilicho na utajo wa Allaah. Ni mamoja ikawa Qur-aan au kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16854
  • Imechapishwa: 17/03/2018